Homa ya mafua ni ugonjwa unasababishwa na kirusi
anaefahamika kwa jina la Influenza ambae hushambulia mfumo wa upumuaji. Homa ya
mafua huenezwa kwa njia ya hewa kupitia kupiga chafya na kukohoa pia
hushambulia sana watoto chini ya miaka mitano, wazee zaidi ya miaka 65, wajawazito na watu wenye
upungufu wa kinga mwilini. Homa huja kwa msimu na msimu wa baridi ndio wakati
wake mwafaka, kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania msimu wa baridi
upo kati ya mwezi Aprili hadi Septemba.
Kwanini Homa ya mafua huenea sana kipindi cha baridi?
Chuo kikuu cha Harvard (moja ya vyuo vikuu bora duniani)
kilichapisha katika tovuti yao nadharia zinazosadifu homa ya mafua kuenea sana
msimu wa baridi:-
- Kirusi aina ya Influenza (anaesababisha Homa ya mafua) hupendelea mazingira ya baridi na makavu, hivyo msimu wa baridi ni msimu mzuri kwake.
- Katika msimu wa baridi watu wengi hupenda kujifungia ndani (kukaa madirisha na milango imefungwa) hivyo husababisha mzunguko mdogo wa hewa ndani ya majengo (kama vile shule, ofisi na nyumba za makazi) pia vyombo vya usafiri (kama vile mabasi daladala n.k) hivyo kurahisisha ueneaji wa virusi vinavyosababisha homa ya mafua.
- Msimu wa baridi jua huonekana muda mfupi sana kwa siku hivyo mwili wa binadamu kushindwa kutengeneza vitamini D (ambayo hutegemea mwanga wa jua kutengenezwa) hii huathiri mfumo wa kinga ya mwili hivyo kushindwa kushambulia virusi vinavyosababisha homa ya mafua.
Unaweza kujitibu homa ya mafua kwa njia za asili kwa
kutumia:-
- Supu ya moto
- Asali
- Tanngawizi ( kwa kuiweka kwenye chai au kuitafuna yenyewe)
(kutoka
tovuti ya Healthline).
KUMBUKA:
- Kupumzika ni jambo la muhimu sana kwa mtu anaeumwa homa ya mafua.
- Kufunika pua na mdomo kwa kitambaa unapopiga chafya na kukohoa.
- Kufanya mazoezi ya mwili ili kuimarisha kinga ya mwili wako.


Nimejifunza kitu
ReplyDelete