Ujasiri ni imani anayokuwa nayo mtu juu ya kufanikiwa kwa
lengo lake. Ujasiri huo unaweza ukawa ni wa kutegemea mtu au ujasiri
binafsi ambao unategemea uwezo wa mhusika katika kutenda jambo flani. Ujasiri
huleta furaha katika maisha na pia
huongeza ufanisi wa kazi unazofanya na pia mahusiano mazuri katika familia na
jamii kwa ujumla.Ktokuwa na ujasiri hupunguza ufanisi wa kazi na huweza
kusababisha msongo wa mawazo.
1.
JITAAMBUE
Jichunguze na uweze kufahamu mambo ambayo
wewe ni dhaifu na mambo yale ambayo wewe
ni hodari unaweza ukayafanya bila wasiwasi. Pia tambua vitu gani unavipenda na vitu gani
unavyovichukia, pia jitambue wewe katika
jamii unatazamwaje na watu na malengo yako kwa ujumla. Hayo yatakusaidia katika
kuepuka mambo yatakayokupa huzuni hivyo kukudhoofisha.
2.
ANZA SIKU YAKO VIZURI
Anza siku yako kwa kufuata ratiba ambayo
umeipangilia na fuata mtiririko wa kazi
au majukumu yako kwa wakati na kwa
ufanisi. Hiyo itakupunguziaz mawazo na kufanya ujione mshindi katika siku hiyo
na kukupa ujasiri waz kufanya majukumu ya kesho.
3.
FANYA MAANDALIZI
Kila jambo unalollipanga katika ratiba
hakikisha mazingira ya kulitekeleza jambo yako sawa na mipango ya awali imekaa
sawa ili kuitiza vizuri ratiba yako na
hivyo kuona umefanikiwa.
4.
JIKUBALI
Kujikubali ni kupuuza madhaifu uliyonayo na
kutumia sehemu ya ubora wako kama
silaha. Kama katika kipengele Fulani uko vizuri sana tumia hicho kipengele
kupanga malengo yako na tumia kama silah
katika maisha yako. Mfano, kama
mtu una kipaji cha uchekeshaji au kucheza mpira au kipaji cha biashara tumia hicho kipajji kama silaha yako ya maisha, utayafunika hata
madhaifu uliyonayo. Amini unaweza katika kila jambo.
5.
PENDA KUJIFUNZA
Pale unapokutana na jambo geni au
shughuli ngeni kwako, uliza kwa watu wengine upate kujifunza au kama ni kazi omba msaada ili upate uzoefu
wa kujaz kufanya kazi hiyo. Hii itakupunguzia makosa katika kazi zako na
kukuongezea uzoefu katika kazi na shughuli tofauti tofauti.
6.
KUWA NA USO WENYE FURAHA
Uso wenye furaha ni silaha kubwa katika
maisha, itakusaidia kukukutanisha na watu
mbalimbali na kukuongezea fursa
za maisha. Pia kuishi na watu vizuri huongezwa na ucheshi na nyuso za
furaha.
7.
FANYA MAMBO MEMA
Wakati
ule unapofanya matendo mabaya dhamira na akili yako huwaz haifikiri
madhara ya baadae. Hivyo penda kujiepusha naz matendo mabaya mapema ikiwemo
marafiki wasioshaurika na makundi mabaya. Hii itakusaidia kuepuka feddheha kwa
jamii naz hivyo kuongeza ujasiri na uaminifu kwa jamii inayokuzunguka.
8.
ACHA MAWAZO MABAYA
Mawazo unayofikiria yana mchango mkubwa
katika maamuzi yako ya mambo mbalimbali, hivyo kuwa na mawzo mabaya
kutakusababishia kutendaz maovu naz
kupoteza mwelekeo wako. Uwaza na kutenda mema roho yako itakuwa na amani
na utakuwa na ujasiri.
9.
TOA MSAMAHA
Kuwa
mwepesi wa kusamehe kutakupunguzia
mawzo mengi yasiyo yaz msingi naz hivyo
kufikiria vizuri juu ya mipango yako na
kuitakeleza kwa ufanisi. Amani ya moyo wako pia inapatikana kwa kusamehe, hivyo
kusamehe kunamsaada mkubwa katika kujiammini kwako.
10.
SAHAU YALIYOPITA
Mambo yaliyopita yote yasahau hii
itakusaidia kupunguza mzigo mkubwa wa kutafakari vipindi vya furaha na huzuni
vilivypita na kukufanya uone bado hujafanya mambo mengi ya muhimu hapa duniani. Mafanikio uliyonayo hutaangalia na
pia mabaya na nyakati za huzuni ulizopitia utazisahau na kuongeza hamasa ya
kutafta zaidi.
Hatua
za kuongeza ujasiri zipo nyingi lakini hizo ni baadhi na unaweza ukazifuata na
kufanikiwa katika malengo yako. Ujasiri ni moja yaz silaha kubwa za maisha ya
mwanadamu
MKUMBUKE
MUUMBA WAKO SIKU ZA UHAI WAKO KABLA MAUTI HAIJAKUKUTA.



Comments
Post a Comment