Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2017

KWANINI HOMA YA MAFUA HUENEA KWA HARAKA MSIMU WA BARIDI?

Homa ya mafua ni ugonjwa unasababishwa na kirusi anaefahamika kwa jina la Influenza ambae hushambulia mfumo wa upumuaji. Homa ya mafua huenezwa kwa njia ya hewa kupitia kupiga chafya na kukohoa pia hushambulia sana watoto chini ya miaka mitano, wazee   zaidi ya miaka 65, wajawazito na watu wenye upungufu wa kinga mwilini. Homa huja kwa msimu na msimu wa baridi ndio wakati wake mwafaka, kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania msimu wa baridi upo kati ya mwezi Aprili hadi Septemba. Kwanini Homa ya mafua huenea sana kipindi cha baridi? Chuo kikuu cha Harvard (moja ya vyuo vikuu bora duniani) kilichapisha katika tovuti yao nadharia zinazosadifu homa ya mafua kuenea sana msimu wa baridi:- Kirusi aina ya Influenza (anaesababisha Homa ya mafua) hupendelea mazingira ya baridi na makavu, hivyo msimu wa baridi ni msimu mzuri kwake. Katika msimu wa baridi watu wengi hupenda kujifungia ndani (kukaa madirisha na milango imefungwa) hivyo husababisha mzunguko mdogo wa hewa...

JOIN US ON TELEGRAM

JOIN US ON TELEGRAM
Join a thousand readers on telegram channel, start a reading habit, get inspired, motivated and learn to win in life.Click on the Image join us