Kughairisha mambo ndio tabia ambayo inaongoza kusababisha watu wengi kutofikia malengo yao kuliko tabia nyingine yeyote, pia tabia ambayo ni ngumu sana kuiacha kama umekwisha kuwa nayo. Kughairisha mambo hutokana na sababu mbalimbali, sababu kuu ikiwa ni kukosa motisha au msukumo wa ndani yako kufanya jambo, pia sababu nyingine kubwa ni kutopangilia mambo yako binafsi. Watu wengi sana huamini kughairisha ni kitu kibaya kabisa katika maisha, jambo ambalo sio kweli. Uzuri au ubaya wa kughairisha hutegemea jambo unaloghairisha, wakati unaoghairisha, na sababu ya kughairisha. Mara nyingi kughairisha hugharimu pale unapoghairisha kwa kutojisikia kufanya jambo bila sababu yoyote (uvivu wa kufanya). Je, unawezaje kupata faida kwa kughairisha? Mwandishi Brian Tracy katika kitabu chake cha Eat that Frog anasema, Kila mtu hughairisha lakini kinachotofautisha kati ya watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa ni katika mambo wanyoghairisha, wengi wasiofanikiwa hughairisha mambo ambayo huc...
Comments
Post a Comment