Kusamehe ni jambo ambao sio rahisi kulifanya hasa pale unapofikiria kuwa aliekukosea amefanya makusudi ili kukuumiza. Lakini ili usiendelee kuumia unatakiwa kufanya jambo moja nalo ni kusamehe. Wengi husamehe lakini baadae huendeleza chuki na hasira juu ya mhusika jambo ambalo sio sahihi, unapotoa msamaha unatakiwa kuondoa hasira na chuki juu ya Yule alie kukosea. Kwakuwa kusamehe ni jambo ambalo huhitaji moyo wenyewe uondoe fikra mbaya zote ulizokuwa nazo juu ya Yule mtu, unaweza kufanya yafuatayo ili uweze kusamehe. 1. ONDOKA ENEO LA TUKIO Kama mtu amekukosea ondoka hiyo sehemu, wakati huo unakuwa na hasira hivyo ukibaki eneo la tukio unaweza kufanya maamuzi ya ajabu. Hivyo kaa mbali ili kupunguza hasira, pata utulivu kwa kufanya jambo unalolipenda mfano:- kusikiliza muziki, kutembea ufukweni au kutulia sehemu unayoona wewe utaweza kutulia. 2. FIKIRIA TUKIO LILIVOKUWA KWA UPANDE WAKO Tuliza akili ...