Habari, najua kama wewe ni kijana kuna wakati unafika unawaza
ni njia gani utumie ili ufikie malengo yako. Kila mtu anawaza kufanikiwa kuwa
na maisha mazuri kujenga familia bora kutunza wazazi wake vizuri n.k. Mafanikio
ya malengo yako hayawezi kupatikana kwa kufanya jambo moja, lazima ufanye mambo
mengi mazuri ili mwisho ufike mahali ambapo ulitarajia kufika. Hapa
nimekuwekea baadhi ya mambo muhimu yanayoweza kuwa na mchango mkubwa katika
safari yako kkuelekea kwenye mafanikio.
Upekee.
Katika dunia ya sasa yenye maendeleo na mapinduzi katika kila
sekta, hakuna kazi au talanta(kipaji) ambacho kina watu wachache kila kazi au
talanta ina watu wengi na ushindani mkubwa. Jambo la pekee linaloweza
kukusaidia kwa sasa ni upekee, fanya kazi au talanta yako lakini kwa ubora na
upekee na ubunifu wa hali ya juu kiasi kwamba utawavutia watu na kushinda
ushindani uliopo. Albert Einstein aliwahi kusema “The woman who follows the
crowd will usually go no further than the crowd. The woman who walks alone is
likely to find herself in place no one has ever been before” (mwanamke
anaefuata kundi hawezi kwenda mbali zaidi ya lile kundi. Mwanamke anaetembea
pekeake anaweza kufika mahali ambapo hakuna mtu aliewahi kufika pale kabla).
Ukitaka kufanikiwa kwa dunia ya sasa lazima ufike mahali ambapo mtu mwingne hajawahi kufika, lakini ukiwa unaiga
na kufuata vitu waanavyofanya watu wengine
huwezi kwenda mbali na kuwazidi wale watu unaowaiga, hivyo huwezi fikia mafanikio.Ukiwa wa pekee utang'ara katika kundi la watu wenye fani, kazi au kipaji kama chako.
Teknolojia.
Kutokana na mapinduzi ya teknolojia watu wengi wanafikiria kwamba huenda itafika kipindi ajira za watu
zitachukuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na teknollojia, lakini ukweli ni
kwamba teknolojia haiwezi kufanya kazi bila kuwepo binadamu.Jambo la kuhofia ni
kwamba mtu ambae hatumii teknolojia
nafasi yake itachukuliwa na mtu anaetumia teknolojia. Kwahiyo jitahidi kwa hali
na mali kuendana au kujua teknolojia na namna unavoweza kuitumia katika fani,
kazi, talanta(kipaji) na katika maisha yako ya kawaida. Teknolojia kwa kizazi
cha sasa na vizazi vijavyo itaendelea kutawala katika kila sekta iwe biashara, elimu, kilimo,afya, viwanda,
michezo. Teknolojia ni nyenzo nzuri sana kwaajili ya mabadiliko chanya ya kazi,
kipaji, elimu na maisha yako endapo
utaamua kuitumia ipasavyo. Tumia teknolojia kung'arisha kazi yako katikati ya ushindani wa watu wanaokuzunguka.
Ushirikiano.
Katika dunia ya sasa yenye kasi ya maendeleo katika kila
sekta, ushirikiano ni jambo la muhimu.
Zamani mtu alikuwa anaweza kujitenga na watu akaishi mbali ilimradi awe na
mahitaji muhimu anaweza akaishi miaka akifanya shughuli zake. Lakini ulimwengu
unabadilika katika kizazi cha sasa ukisikia mtu amefanikiwa kimaisha basi kuna
watu ameshirikiana nao. Chagua watu wenye maono
ya mbali, wenye ndoto za maisha watakaokupa morali ya kutafuta maisha
kwa nguvu na akili zako zote. Marafiki sio lazima wawe ni watu ambao wapo na
wewe kwenye kazi, biashara, au fani moja, inawezekana pia ukawa na marafiki
wanaofanya shughuli tofauti na wewe ilimradi mnashirikiana katika kutafuta
maisha na kusaidiana katika nyakati tofauti tofauti. Marafiki ni moja ya kitu muhimu katika maisha vitu vingine ni Mwenyezi
Mungu na Familia.
Muda.
Hili ni jambo ambalo
tunakumbushwa mara kwa mara kwamba muda
ni mali. Katika ulimwengu wa
sasa kila kitu kinaenda kasi sana hivyo
katika kupambana na maisha kumbuka kupambana na muda pia, utafika wakati wa
kuoa au kuolewa au wakati ambao wale uliokuwa unawategemea (wazazi au walezi)
wanakuwa tegemezi kwako, majukumu yanaongezeka wakati huo malengo yako
hayajatimia lazima ukwame. Kwahiyo kuendana na majira na wakati pia ni jambo la
muhimu sana katika maisha ya leo. Ukiweza kujua na ukafanya kila jambo kwa
wakati wake utaona namna malengo yako yanaendana.
Kujifunza.
Kujifunza sio kusoma pekee, katika suala la kujifunza kuna
namna nyingi za kujifunza wengi wetu tunajali zaidi kujifunza kupitia taasisi
za elimu au kwa watu waliofanikiwa. Lakini unaweza kujifunza kwa rafiki,
wasiliana na rafiki yako muulize “jambo
Fulani wewe huwa unatumia njia ipi kulifanya na unatumia muda gani?” akikujibu
linganisha na namna wewe unavofanya angalia njia ipi ni rahisi inayotumia muda
mfupi na kuleta matunda/matokeo mazuri. Unaweza kujifunza pia kwa kutembelea
mahali mbali na mazingira yako ukaona namna watu wa eneo lile namna wanavofanya
shughuli zao linaganisha na namna mnavofnya katika mazingira yako na utajifunza kitu tofauti. Tumia siku
za mwisho wa wiki (weekend) kutembelea maeneo tofauti uone vijana wenzio
wanatafutaje riziki.
Tahadhari.
Katika safari yako haijalishi umbali gani umeenda katika njia
isiyo sahihi, unatakiwa utafute njia
sahihi punde tu unapotambua kuwa unapotea. Tahadhari ni jambo la muhimu sana
katika maisha linakufanya unakuwa makini katikka kila jambo unalofanya. Dunia
kwa sasa kutokana na utandawazi kikla jambo linaenda kwa kasi sana ukifikiria
kufanya jambo hakikisha unalifanya kwa wakati, ukifikiria wazo zuri au fursa mpya ukabaki nayo kichwani keshokkutwa
utakuta kuna mtu ameshatumia hiyo fursa na ameshasogeza hatua mbele. Pia ukiona
azu kusikia fursa Fulani ina faida kubwa ifanye kwa tahadhari kwa kuangalia
mbeleni, unaweza kuona leo kitu Fulani kinaweza kukupa faida au kukusogeza
kimaisha lakini kutokana na maisha yanavoenda kasi kesho hilo jambo azu fursa
ikawa imepitwa na wakati. Hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari mapema, ukiwa na
fursa zaidi ya moja jitahidi kulinganisha kwa umakini na uhakika ili kufanya
jambo lenye tija mbeleni.
Napenda kukumbusha kwamba mafanikio sio jambo lialokuja
haraka kulala na unaamka umefanikiwa au unafanya jambo moja unafanikiwa. Lazima
ufanye mambo mengi upitie vipindi tofauti tofauti shida raha na mateso
ukivumilia nyakati zote hizo mwisho utafikia malengo.






Comments
Post a Comment