Kila mchoraji kabla ya kuchora picha huwa na taswira ya picha hiyo akilini mwake, kisha huamua kubadili taswira ile kuwa mchoro. Ndivyo yalivyo maisha yetu ya kila siku, akilini mwako unakuwa na ndoto nyingi za maisha ambazo kwa muda huo ni taswira tu iliyopo akilini mwako unahitaji kuamua na kuchukua vifaa na zana na kuanza kubadili taswira hiyo kuwa mchoro halisi yaani upange mipango na kuitekeleza ili ufikie ndoto zako za kimaisha. Kila mtu akilini mwake ana taswira ya pekee ya maisha anayoyapanga na kuyapigania ili ayafikie. Kama ilivyo kwamba mchoraji hawezi kuwa na taswira au kuchora kituambacho hajawahi kusikia wala kuona vivyo hivyo katika maisha ya binadamu taswira ya maisha yako hujengwa na taarifa unazozijua au kuzisikia kuhusu maisha. Ubora wa taswira uliyonayo kichwani hutegemea taarifa ulizonazo juu ya maisha kama una taarifa sahihi kuhusu maisha basi akili yako pia itajenga taswira bora ya maisha na vivyo hivyo hujenga taswira isiyo na ubora kama huna taarifa za...