Kila jambo unalolifanya duniani linakuwa na asilimia kadhaa ya kushindwa, ndio maana watu huwa na plani B. Unaweza kufanya jambo kwa uhakika kabisa lakini kitu kidogo sana kikakufanya ushindwe, na hii ndio inafanya watu wafanye vitu kwa umakini na kufikiria sana hasa pale ambapo unania ya kufanikiwa katika mambo yako. Lakini muda mwingine unaweza kuwa umefanya jambo kwa umakini sana bila kukosea lakini ukashindwa kwasababu za mtu mwingine ambae mlikuwa mnashirikiana nae huenda ni kwa uzembe au bahati mbaya lakini mambo ndio yameharibika. Lawama Katika hali kama hii ndipo watu huanza kutupiana lawama, huyu anamwambia mwingine “Unaona uzembe wako umetutia hasara”, Yule pia anatafuta sababu ya yeye kukosea, anaweza akatupia mpira kwa mwingine au la akalaumu vifaa alivyotumia au miundombinu, ilimradi asionekane mkosaji. Katika kampuni au madaraka Fulani watu hupenda kuwatupia lawama watu wa chini yao kimadaraka, lawama hizi huenda ngazi kwa ngazi mpaka kumfikia mtu wa ...