Skip to main content

KUGHAIRISHA KWENYE FAIDA


Kughairisha mambo ndio tabia ambayo inaongoza kusababisha watu wengi kutofikia malengo yao kuliko tabia nyingine yeyote, pia tabia ambayo ni ngumu sana kuiacha kama umekwisha kuwa nayo. Kughairisha mambo hutokana na sababu mbalimbali, sababu kuu ikiwa ni kukosa motisha au msukumo wa ndani yako kufanya jambo, pia sababu nyingine kubwa ni kutopangilia mambo yako binafsi.
Watu wengi sana huamini kughairisha ni kitu kibaya kabisa katika maisha, jambo ambalo sio kweli. Uzuri au ubaya wa kughairisha hutegemea jambo unaloghairisha, wakati unaoghairisha, na sababu ya kughairisha. Mara nyingi kughairisha hugharimu pale unapoghairisha kwa kutojisikia kufanya jambo bila sababu yoyote (uvivu wa kufanya).
Je, unawezaje kupata faida kwa kughairisha?
Mwandishi Brian Tracy katika kitabu chake cha Eat that Frog anasema, Kila mtu hughairisha lakini kinachotofautisha kati ya watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa ni katika mambo wanyoghairisha, wengi wasiofanikiwa hughairisha mambo ambayo huchangia 80% ya maisha yao, wakati wale wanaofanikiwa hughairisha mambo ambayo huchangia 20% katika maisha yao.
Mara nyingi mambo amabayo ni ya muhimu sana huwa na vikwazo na ugumu katika kuyafanya hivyo usipokuwa na msukumo kutoka ndani ya nafsi yako ni rahisi kughaili na kukimbilia katika mambo ambayo yana umhimu kidogo katika maisha yako na mara nyingi mambo haya huwa rahisi na yasiyo na vikwazo katika kuyafanya.
Ili uweze kutumia kughairisha kwenye faida katika maisha yako ya kila siku kwanza unahitaji mambo yafuatayo:- 

  • UTAMBUA MAMBO MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO.
Jitambue kwanza wewe ni nani? Lengo lako hapa duniani ni lipi? Na unaelekea wapi?
Kisha orodhesha mambo/shughuli za muhimu ambazo zitakufikisha zitakupeleka huko unakotaka kufika. Mambo ambayo yanachangia asilimia 80 ya maisha unayotaka kuyaishi hayo ndio mambo muhimu, haya ni mambo ambayo ni ya kuyapa vipaumbele ukilinganisha na mambo mengine.

  • RATIBA YA SHUGHULI ZAKO ZOTE.
Kuwa na ratiba ya shughuli zote unazohitaji kuzifanya katika siku, wiki na mwezi. Ukishaziorodhesha shughuli zote, unatakiwa kuzipanga shughuli hizo kwa mtiririko kulingana na umuhimu, uhitaji na uharaka wa shughuli hizo. Shughuli za muhimu na ambazo zinahitajika kukamilisha haraka zikae mwanzoni na zile ambazo hata ukikosa muda unaweza kufanya siku inayofuata zikae mwishoni mwa orodha.



  • KUWA NA UTARATIBU MAALUMU WA KUPOKEA MAMBO.
Je, ukipewa taarifa au jukumu la kufanya ambalo hukuliweka kwenye ratiba unafanyaje? Au rafiki yako akikupa taariafa ya kukutembelea ghafla unafanyaje? Lazima uwe na utaratibu maalumu ambao hata watu wengine yaani ndugu, jamaa na rafiki wanatambua kuwa nikitaka kumfuata Fulani natakiwa kufanya hivi kabla. Kwa kifupi usiwe mtu wa ndio kila wakati. Kwa upande wa dharura ambazo ni za muhimu sana lazima uwe na uratibu wake pia. Ni kawaida katika maisha kutokea dharura na mara nyingi dharura hutukuta tukiwa hatujajiandaa, lakini pia ni muhimu kupima dharura hizo hivyo unatakiwa kuwa na utaratibu maalumu wa kupokea.

Hivyo katika kughairisha kwenye faida, ukiwa na mambo mawili au zaidi ambayo yanahitajika kufanyika kwa wakati mmoja, kitu cha kwanza unaangalia je lipi ni jambo ambalo ni muhimu zaidi kwako?, cha pili ni je jambo lipi liko kwenye ratiba yako? (Kati ya lile lililopo kwenye ratiba na lile lililokujia kama dharura lipi la muhimu zaidi kwako katika maisha), cha tatu je, utaratibu wako wa kupokea jambo kama hilo ni upi?

Unaweza kughairisha kwenda matembezini kwasababu rafiki yako amekuja na anataka msome pamoja kitabu kipya alichokuletea, Lakini pia mwingine anaweza kutokughairisha kwenda matembezini kwasababu anaenda kufanya utafiti wa biashara mpya katika matembezi yake, hivyo akamkatalia rafiki yake kwakuwa kusoma kitabu hakukuwa kwenye ratiba yake.

Maisha ni jinsi wewe mwenyewe unavyoyapangilia na kuyaishi.

Kila la kheri katika shughuli zako za kila siku,
USICHOKE KUJIFUNZA.

Comments

Popular posts from this blog

HATUA 10 ZA KUONGEZA UJASIRI BINAFSI

 Ujasiri ni imani anayokuwa nayo mtu juu ya kufanikiwa kwa lengo lake. Ujasiri huo unaweza ukawa ni wa kutegemea mtu au ujasiri binafsi  ambao unategemea  uwezo wa mhusika katika kutenda jambo flani. Ujasiri huleta furaha katika maisha na  pia huongeza ufanisi wa kazi unazofanya na pia mahusiano mazuri katika familia na jamii kwa ujumla.Ktokuwa na ujasiri hupunguza ufanisi wa kazi na huweza kusababisha msongo wa mawazo. 1.        JITAAMBUE Jichunguze na uweze kufahamu mambo ambayo wewe ni dhaifu na mambo yale ambayo wewe  ni hodari unaweza ukayafanya bila wasiwasi. Pia tambua  vitu gani unavipenda na vitu gani unavyovichukia, pia jitambue  wewe katika jamii unatazamwaje na watu na malengo yako kwa ujumla. Hayo yatakusaidia katika kuepuka mambo yatakayokupa huzuni hivyo kukudhoofisha. 2.        ANZA SIKU YAKO VIZURI Anza siku yako kwa kufuata ratiba ambayo umeipangilia na fuata...

MAMBO MUHIMU KWAKO KIJANA WA LEO.

Habari, najua kama wewe ni kijana kuna wakati unafika unawaza ni njia gani utumie ili ufikie malengo yako. Kila mtu anawaza kufanikiwa kuwa na maisha mazuri kujenga familia bora kutunza wazazi wake vizuri n.k. Mafanikio ya malengo yako hayawezi kupatikana kwa kufanya jambo moja, lazima ufanye mambo mengi mazuri ili mwisho ufike mahali ambapo ulitarajia kufika. Hapa nimekuwekea baadhi ya mambo muhimu yanayoweza kuwa na mchango mkubwa katika safari yako kkuelekea kwenye mafanikio. Upekee. Katika dunia ya sasa yenye maendeleo na mapinduzi katika kila sekta, hakuna kazi au talanta(kipaji) ambacho kina watu wachache kila kazi au talanta ina watu wengi na ushindani mkubwa. Jambo la pekee linaloweza kukusaidia kwa sasa ni upekee, fanya kazi au talanta yako lakini kwa ubora na upekee na ubunifu wa hali ya juu kiasi kwamba utawavutia watu na kushinda ushindani uliopo. Albert Einstein aliwahi kusema “The woman who follows the crowd will usually go no further than the crowd. The woman who wa...

50 REASONS TO READ BOOKS FROM SPEAKING TREE BLOG

Join more than a thousand readers 1. Books help to feel more confident. 2. Books help to travel around the world in the cheapest way. 3. Books develop your personality. 4. Books provide food for thought. 5. Books make you laugh and think. 6. Books draw you towards perfection. 7. Books stimulate creativity. 8. Books bring out writing talent. 9. Books help in communicating. 10. Books clear your vision. 11. Books satisfy your curiosity. 12. Books help you make more choices. 13. Books help you build literary talent. 14. Books do not require any special device to teach. 15. Books increase your attention span. 16. Books are fruitful pastime. 17. Books can be used anytime, anywhere. 18. Books provide entertainment, when others fail. 19. Books make you powerful. 20. Books help you know the 'Whys' and 'Hows' of everything. 21. Books help you to create and spread fun. 22. Books help you travel across time intelligently. 23. Books keep you updated with f...

SILAHA YA KUTOLAUMU KUFIKIA MAFANIKIO.

Kila jambo unalolifanya duniani linakuwa na asilimia kadhaa ya kushindwa, ndio maana watu huwa na plani B. Unaweza kufanya jambo kwa uhakika kabisa lakini kitu kidogo sana kikakufanya ushindwe, na hii ndio inafanya watu wafanye vitu kwa umakini na kufikiria sana hasa pale ambapo unania ya kufanikiwa katika mambo yako. Lakini muda mwingine unaweza kuwa umefanya jambo kwa umakini sana bila kukosea lakini ukashindwa kwasababu za mtu mwingine ambae mlikuwa mnashirikiana nae huenda ni kwa uzembe au bahati mbaya lakini mambo ndio yameharibika.  Lawama Katika hali kama hii ndipo watu huanza kutupiana lawama, huyu anamwambia mwingine “Unaona uzembe wako umetutia hasara”, Yule pia anatafuta sababu ya yeye kukosea, anaweza akatupia mpira kwa mwingine au la akalaumu vifaa alivyotumia au miundombinu, ilimradi asionekane mkosaji. Katika kampuni au madaraka Fulani watu hupenda kuwatupia lawama watu wa chini yao kimadaraka, lawama hizi huenda ngazi kwa ngazi mpaka kumfikia mtu wa ...

JOIN US ON TELEGRAM

JOIN US ON TELEGRAM
Join a thousand readers on telegram channel, start a reading habit, get inspired, motivated and learn to win in life.Click on the Image join us