Kusamehe ni kitendo cha kuondoa hasira, maumivu na hisia
unazokuwa nazo baada ya kukosewa. Kila binadamu anapokosewa huona ameonewa na
sio haki kile alichofanyiwa hivyo huwa na hasira na hisia za maumivu. Kila lile
jambo au tendo linapojirudia akilini mwake hupata maumivu moyoni, hukosa furaha
amani na hata kupata msongo wa mawazo.
Njia ya kuondokana na maumivu hasira na mawazo yote ni
kusamehe. Hapa ndipo wengi huona ni jambo gumu, pale ambapo mtu amekukosea sana
halafu wewe uje umsamehe kirahisi tu. Wengi huona sio haki na kuchukua uamuzi
wa kulipiza kisasi. Yafahamu haya kuhusu kusamehe:-

1. KUSAMEHE NI
KUJIPENDA MWENYEWE
Unapotoa msamaha unaondoa hasira maumivu na mawazo
yote uliyonayo juu ya Yule mtu alie kukosea, hivyo kuweka huru moyo wako na
akili yako. Kubaki na hasira, maumivu na
hasira ni hasara kwako kwani huhatarisha afya yako.
2. USISUBIRI
MPAKA UOMBWE MSAMAHA
Watu wengi kusamehe mpaka waombwe msamaha, hilo
halifai fikiria Yule aliekukosea asipokuomba msamaha utaendelea kuteseka na mawazo mabaya na
kutawaliwa na hasira mpaka lini?. Jambo la muhimu ni kusamehe hata kama
hujaombwa msamaha maana ni faida kwako mwenyewe.

3. KUSAMEHE
SIO UJINGA
Mtu anaposamehe wengi hufikiria ni ujinga hasa vijana
wa leo, pale mtu anapokukosea kosa kubwa halafu wanaona umemsamehe wao huona ni
ujinga. Utwasikia wakisema “Ningekuwa mimi nisingemsamehe, ujinga huo” lakini
ni kwasababu hawajui faida za kusamehe. Anaesamehe ana faida nyingi kuliko
anaesamehewa.
4. KUSAMEHE
SIO UNYONGE
Pale inapotokea mkubwa wako amekukosea na ukamsamehe
hata kabla hajakuomba msamaha, watu wengi hufikiria kuwa umemsamehe kwakuw wewe
ni mnyonge kwake, jambo ambalo si
sahihi. Kusamehe ni jambo la kishujaa na
ndio maana ni watu wachache wenye uwezo wa kusamehe, wengi katika
nyakati za sasa hulipiza kisasii kwa kuwa ni wadhaifu mioyoni mwao (jambo wana
nguvu za miili), hivyo hushindwa kusamehe.
5. SIO LAZIMA
KURUDISHA UHUSIANO WENU WA ZAMANI
Kama rafiki yako wa karibu amekusaliti kiasi cha
kukuumiza moyo wako, ukimsamehe mnaweza mkarudisha urafiki wenu au msiurudishe.
Pale ambapo unaona rafiki yako hatambui makosa aliyoyafanya na hana wasiwasi
wala woga juu ya hilo, unaweza ukamsamehe halafu kila mtu akaishi maisha yake
kwa amani.
6. NI NJIA YA
KUTAFUTA AMANI YA MOYO WAKO
Moyo wako ukiwa na msongo wa mawazo ni mateso sana
kwako, hivyo samehe ili upate amani ya moyo na kuwa na utulivu akilini mwako
hivyo kuendelea na kazi na mmipango yako kwa
amani na furaha.
7. KUSAMEHE
SIO JAMBO RAHISI
Kumsamehe mtu aliekukosea kunahitaji kujitoa moyoni
kwani tukio huendelea kujirudia akilini mwako hivyo kurejesha kumbumbu za
hasira na maumivu. Kusamehe kunahitaji utulivu wa kufikiria jambo na busara
kukusaidia kutoa msamaha wa kweli.
Kusamehe ni
ushujaa na ni watu wachache wenye uwezo wa kusamehe.

Dunia ingekuwa ni sehemu nzuri ya furaha kama kila
mmoja angekuwa anasamehe, kwani matukio mengi mabaya kwa sasa ni kulipiza
kisasi. Jiepushe na kutenda makosa na
mtu akikukosea toa msamaha. Hiyo ni njia ya kuweka mahusiano mazuri ya kiimani
katika dini
ANZA KUWA
NA MAZOEA YA KUSAMEHE, MWISHO ITAKUWA NI UTARATIBU WAKO.
Comments
Post a Comment