Kusamehe ni jambo ambao sio rahisi kulifanya hasa pale
unapofikiria kuwa aliekukosea amefanya makusudi ili kukuumiza. Lakini ili
usiendelee kuumia unatakiwa kufanya jambo moja nalo ni kusamehe. Wengi husamehe
lakini baadae huendeleza chuki na hasira juu ya mhusika jambo ambalo sio
sahihi, unapotoa msamaha unatakiwa kuondoa hasira na chuki juu ya Yule alie
kukosea. Kwakuwa kusamehe ni jambo
ambalo huhitaji moyo wenyewe uondoe fikra mbaya zote ulizokuwa nazo juu ya Yule
mtu, unaweza kufanya yafuatayo ili uweze kusamehe.
1. ONDOKA ENEO
LA TUKIO
Kama mtu amekukosea ondoka hiyo sehemu, wakati huo
unakuwa na hasira hivyo ukibaki eneo la tukio unaweza kufanya
maamuzi ya ajabu. Hivyo kaa mbali ili kupunguza hasira, pata utulivu kwa
kufanya jambo unalolipenda mfano:- kusikiliza muziki, kutembea ufukweni au
kutulia sehemu unayoona wewe utaweza kutulia.

2. FIKIRIA
TUKIO LILIVOKUWA KWA UPANDE WAKO
Tuliza akili yako na ufikirie vizuri kosa kwa marefu
na mapana, anza kufikiria kama kosa umelifannya wewe ungelichukuliaje. Jaribu
kuchukua nafasi zote, nafasi ya mkosaji na nafasi ya aliekosewa ambayo wewe
ndio mhusika mkuu ili uweze kulichambua vizuri kosa hilo.
3. FIKIRIA
KUWA WEWE PIA NI MKOSAJI
Fikiria pia kuwa wewe ni mkosaji, hivyo jaribu
kukumbuka makosa ambayo umewahi kuyafanya na ukasamehewa hivyo unastahili kusamehe pia. Ukilitambua
hilo utaweza kuona hitaji la kumsamehe mkosaji.
Baada ya hapo utaweza kuondoa kinyongo juu ya mkosaji na
utatoa msamaha na kuwa ni amani.
Kumbuka
kutoa msamaha ni kwa faida yako, na hilo ni jambo la msingi kwa afya na maisha
yako kwa ujumla.
Kumbe una blog na ww
ReplyDelete