Siku zote tumezoea kusikia majina ya watangazaji redioni na
hata kwenye televisheni kwa kuwa wao ndio wana uhusiano wa moja kwa moja na hadhira
(wasikilizaji na watazamaji), lakini nani amezoea kusikia majina ya mafundi
mitambo au wachukua picha (camera man)? Ni nadra sana kusikia majina ya hawa
watu, japo nao wana mchango mkubwa katika kufikisha matangazo yale kwa hadhira.
Hivyo ndivyo ilivo hata kwa wazazi wetu, mama ni mzazi ambae
mda wote yupo karibu na mtoto na huduma nyingi mtoto anazipata toka kwa mama na baba ni mtu wa mihangaiko huonana na watoto mara chache zaidi kuliko mama,
lakini hii haina maana kwamba baba hahusiki kwenye malezi ya huyu mtoto la
hasha ila analea kupitia mgongo wa mama.
Mtoto anajua kila kitu analeta mama kwakuwa haoni huduma za
baba, lakini tambua kwamba huo uji anaokupikia mama ni baba alietafuta unga. Ni
kweli mda mwingine mzazi mmoja anakuwa mzembe katika majukumu, hilo lipo kwa
pande zote mama na hata baba anaweza akatelekeza watoto wake
Leo kila mtu anasema nani kama mama ni kweli upo sahihi
lakini sijawahi kuona mtu akimshukuru baba kwenye mitandao ya kijamii,
unafikiri wakati mama yako anatunza mimba yako baba alikuwa anastarehe?. Hufikirii
kuwa hata mama yako alikuwa msumbufu kwa baba kutokana na mabadiliko ya mwili
wa mama mjamzito. Kuna mambo mengi baba kafanya mpaka leo wewe uko hapo aidha amemfanyia mama wewe ukiwa tumboni mwake au amefanya ukiwa umezaliwa. Hebu
uwe na heshima kwa wazazi wote hata unapowashukuru washukuru wote kwa pamoja.
WAZAZI WOTE NI SAWA.
Hakuna mzazi anaejisikia vizuri kuona mzazi mwenzake anapokea
shukrani halafu yeye hapewi na mtoto ambae wammelea wote.
Mimi nakusihi waheshimu wazazi wote, maana kuna watu
wanamheshimu baba na mama wanamdharau, mara nyingi hutokana na upole wa mama na wengi humuheshimu baba hata kutetemeka anapoongea nao, ila utaona mitandaoni wanapost nani kama
mama.
NANI KAMA MAMA WAKATI HUMHESHIMU NA HUMSIKILIZI KAMA UMSIKILIZAVYO NA KUMHESHIMU BABA?.
NANI KAMA MAMA WAKATI HUMHESHIMU NA HUMSIKILIZI KAMA UMSIKILIZAVYO NA KUMHESHIMU BABA?.
NAKUPENDA MAMA NA BABA



Comments
Post a Comment